![]() |
| Boniface Wambura |
Mwandishi wetu
WAKATI uongozi wa Yanga ukiitaka Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kuwaomba radhi kutokana na kutowatumia mwaliko katika hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki Ligi Kuu, bodi hiyo imefanya hivyo.
Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema jana walishindwa kwenda katika hafla ya utoaji vifaa kwa kuwa hawakupata mwaliko kutoka TFF na Bodi ya Ligi.
''Yanga mbali ya kuwa klabu kubwa pia ni mabinga watetezi wa Ligi ya Vodacom, ilipaswa kutumia mwaliko mapema na si siku moja kabla ya tukio.''
Akizungumzia tukio hilo jana , Mtendaji Mkuu wa Bondi ya Ligi, Boniface Wambura alisema wanaomba radhi kutokana na kuchelewa kupeleka mwaliko kwa njia ya mtandao.
Kiungweana tunaitaka radhi Yanga, ingawa hata viongozi wengine waliofika kwenye hafala ya kukabidhi vifaa walikuja baada ya kuona mwaliako kwenye mtandao, njia ambayo tumekuwa tukiitumia mara kwa mara.
Katika hafla ya utoaji jezi iliyofanyika jana Dar es Salaam, Yanga haikuwa na mwakilishi, kitu kilichoifanya Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kujiokeza kupokea jezi kwa niaba yao, huku akipiga kijembe kuwa wamekuwa na tabia ya kuchelewa chelewa katika matukio.
Wakati akitoa kijembe hicho Simba nayo haikutokea katika hafla ya kukabidhi zawadi wa washindi wa Ligi Kuu ya Vodadom 2016-17.
Simba ilishika nafasi ya pili nyuma ya Yanga iliyotwaa ubingwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga. Pia Mchezaji Bora wa ligi alitoka kweny klabu yao, Mohammed Hussein 'Tshabalala'.

Comments
Post a Comment