Skip to main content

BIKO yajitosa udhamini Stand United


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele , aliyetafuta udhamini wa BIKO kwa Stand United.
TIMU ya Stand United ‘Chama la Wana’ imeangukiwa na zali la mentali (bahati) kwa kupata udhamini wa mwaka mmoja uliotolewa na BIKO ambayo ni  Kampuni inayojishulisha na michezo ya bahati nasibu mtandaoni.

Udhamini huo wa shilingi milioni 100 ni wa msimu wa 2017-2018.

Kwa kupata udhamini huo ni habari njema kwa Stand United ambayo, ilikumbwa na matatizo ya kifedha msimu uliopita baada ya Agosti 2015 kupata udhamini wa miaka  mwili kutoka  kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA Mining wenye thamani ya bilioni 2.4, lakini ulivunjika kutokana na viongozi wa klabu hiyo kutofautiana

Stand yenye maskani yake Shinyanga, imepata udhamini huo katika wakati mzuri ambapo leo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017-2018 inaanza rasmi.

Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United,Dkt. Ellyson Maeja .
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kama Ijumaa,Agosti 25,2017mjini Shinyanga, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele (CCM) alisema BIKO wameidhamini timu hiyo baada ya kuridhishwa na mwenendo wake.

Katika msimu uliopita Standi ilimaliza Ligi Kuu ikiwa katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu, timu hiyo ilianza vizuri msimu ikiwa chini ya Kocha mfaransa, Patrick Liewig lakini ilizurota katika mzunguko wa pili wa Ligi baada ya kocha huyo kuondoka, kitendo kilichochangiwa na kuvunjika kwa mkataba wa Acacia ambayo ilikuwa ikimlipa mshahara.

“Baada ya Stand United kupoteza mwelekeo na wadhamini wake Kampuni ya Acacia kujiondoa katika udhamini,hivi sasa nimeamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hii, nimetafuta udhamini mwingine, nimeiomba kampuni ya Kitanzania ya BIKO ,imekubali kuwa wadhamini wakuu kwa mwaka mmoja  na imetupatia shilingi milioni 100 kwa mwaka huu”,alisema Masele ambaye pia ndiye aliyetafuta udhamini wa Acacia .

Masele aliwatahadharisha viongozi wasifanye matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na wadhamini hao na kuongeza hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United,Dkt. Ellyson Maeja alisemayao imejipanga vizuri kuhakikisha  inafanya vizuri  ligi ya msimu  huu.

“Timu yetu kwa sasa imetulia kiuongozi, tatizo ni bajeti, mpira ni pesa, bila pesa hakuna timu, lakini pia hatuna usafiri wala hosteli kwa ajili ya wachezaji, tunaomba wadau waendelee kujitokeza kuisaidia timu hii, tumesajili wachezaji wapya 19, jumla wako 30, tunaye kocha mzuri, walimu wazuri, malengo yetu ni kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu wa 2017-2018,″ alisema Dkt.Maeja.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...