![]() |
| Wachezaji wa timu za Barcelona na Chapecoense wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao wa kuwania kombe la Joan Gamper jana. |
BARCELONA , Hispania
TIMU ya Barcelona imeifunga Chapecoense ya Brazil ambayo Novemba mwaka jana ilipoteza wachezaji wake wengi katika ajali ya ndege iliyotokea nchini Colombia.
Katika mchezo huyo uliofanyika jana Camp Nou, haikuwa ni Lionel Messi ambaye alishangiliwa sana na wala haikuwa kama Neymar alivyowahi kushangiliwa alivyotambulishwa, ambaye amehamia Paris Saint-Germain wiki iliyopita.
Badala yake, walikuwa wachezaji kutoka nchi moja na Neymar wa timu ya, Chapecoense, ambayo iliialikwa na Barcelona katika mchezo wa kuwania kombe la Joan Gamper , ambao hufanyika kukaribisha msimu mpya.
Ajali hiyo ilitokea Novemba 29, mwaka jana wakati Chapecoense ilipokuwa safarini kwenda Colombia kupambana na Atletico Nacional katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Copa Sudamericana. Wachezaji 19 na wafanyakazi walifariki, ni wachezaji watatu tu walinusurika .
Kutokana na kuangamia kwa wachezaji 19 wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo, klabu kubwa za Brazil na Argentina zilijitolea kutoa wachezaji kwa mkopo kwa Chapocense, ambayo iliwasaini wapya 25 na kuwapandisha tisa kutoka timu ya vijana.
Timu ya Barcelona pamoja na kukubaliwa kucheza mchezo huo, imetoa mchango wa euro
250,000 (zaidi ya sh. milioni 660) kwa Chapecoense.
Pamoja na kushangilia kabla ya mchezo kuanza kulikuwa na hali ya simanzi katika uwanja wa Camp Nou baada ya kujitokeza wachezaji watatu ambao walinusurika katika ajali hiyo ya ndege.
![]() |
| Wachezaji watatu wa timu ya Chapecoens walionusurika katika ajali ya ndege. Kutoka kushoto ni Jakson Follmann, Neto na Alan Ruschel walipotambulishwa kabla ya mchezo dhidi ya Barcelona |
Wachezaji walionusurika waliotambulishwa ni Alan Ruschel, Neto na Jackson Follmann.
Alan ambaye alikuwa nahodha wa Chapecoense, alicheza mechi yake ya kwanza tangu ilipotokea ajali hiyo mbaya Novemba .
Neto, amekwua an matumaini ya kucheza tena, lakini Follmann ndoto zake za kucheza soka ya kulipwa imeisha kutokana na kukatwa mguu wake mmoja na anatembea kwa msaada wa chuma .
Kwa heshima wachezaji wawili walionusurika walipewa heshima ya kupiga mpira kabla ya mchezo kuanza na wakatoka nje ya uwanja, wachezaji wa timu hiyo walivaa jezi zenye rangi ya kijani na nyeupe.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki 64,705, mabao ya Barceliona yalifungwa na Messi, Gerard Deulofeu, Sergio Busquets, Luis Suarez na Denis Suarez .
Ndani ya dakika nne, Barce inayonolewa na Kocha Ernesto Valverde ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 mabao hayo yalifungwa katika dakika 12 za kwanza.
Barca ilitumia mchezo huo kwa maandalizi kabla ya mchezo dhidi ya mahasimu wao Real Madrid wa kuwania Kombe la Hispania (Super Cup) Jumapili Agosti 13, mwaka huu.


Comments
Post a Comment