Gareth Bale akimruka mlindamlango Deportivo, Ruben Martinez.
TIMU za Barcelona na Real Madrid zimeibuka na ushindi katika michezo yao ya kwanza ya La Liga msimu huu dhidi ya timu za Real Betis na Deportivo La Coruna.
Barcelona ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Real Betis 2-0 katika uwanja wa Nou Camp,ukiwa ni mchezo wao wa kwanza tangu kutokea mashambulio ya kutisha la kigaidi katika mji mkuu wa Catalan na Cambrils.
Real Madrid imeanza kampeni yake ya kutetea ubingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008 kwa ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna, huku Sergio Ramos akitolewa kwa kadi nyekundu katika sekunde za mwisho.
Mlinzi wa Betis, Alin Tosca alijifunga wakati akiwa kwenye jitihaza za kuokoa mpira wa krosi kutoka kwa Gerard Deulofeu wa Barcelona dakika ya 36, huku mshambuliaji wa zamani wa Everton aliyerusi katika timu yake aliyoichezea utotoni pia alitoa pasi ya bao la pili kwa
Sergi Roberto dakika ya 39.
![]() |
| Wachezaji wa Barcelona wakipongezana baada ya kupata bao |
Katika mchezo huo, Lionel Messi alikuwa na mzigo mzito wa kuongoza safu ya ushambuliaji kutokana na kutowepo Luis Suarez na Andres Iniesta, hakufunga bao lakini aligongesha mwamba mara tatu.
Gareth Bale alifunga bao la kwanza kwa Madrid dakika ya 20 kabla ya Casemiro kuongeza la pili dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho .
Toni Kroos kisha alikutana mpira kutoka kwa Bale na kufunga bao la tatu kwa Real dakika ya 62 , kabla ya Ramos kuoneshwa kadi ya pili ya njano katika muda wa majeruhi.


Comments
Post a Comment