![]() |
| Abdi Banda |
MLINZI wa zamani wa Simba, Abdi Banda amefunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) kuinusuru timu yake ya Baroka Swallows kufungwa dhidi ya Orlando Pirates inayonolewa na Kocha wa zamani wa Yanga na Uganda, Mserbia, Sredojevic Milutin maarufu kama Micho.
Baroka FC waliokuwa nyumbani, walianza kufungwa bao dakika ya 41 kwa bao la Thabo Qalinge na kufanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Banda aliyekuwa alikuwa kinara katika safu ya ulinzi alifunga bao la kusawazisha dakika ya 73.
Kwa kufunga bao hilo inaonesha Banda ameanza kujenga imani kubwa kwa kocha wake Kgoloko Thobejane kuzidi kumtumia kwenye mipango yake.

Comments
Post a Comment