![]() |
| Wachezaji wa timu ya Azam FC wakipasha miili. |
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itacheza mechi nne za kirafiki nchini uganda ambako imeweka kambi ya siku 10, kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2017-18.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu hiyo, jumla ya timu nne zimethibitisha kucheza na Azam FC, timu ya mwisho ikiwa ni Vipers ambayo watacheza nayo katika jiji la Kampara Agosti 11 mwaka huu.
Timu nyingine zilizothibitisha awali ni KCCA mchezo utakaofanyika keshokutwa Alhamisi saa 10.00 jioni, ukifuatiwa na huo wa Vipers Agosti 11, Ondurapaka Agosti 13 kabla ya kkumaliza ziara kwa kupambana na URA Agosti 14.
Azam ilikwenda Uganda Agosti 6, mwaka huu, Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, anaamini kikosi chake kitanufaika kwa kambi hiyo ya siku 10 nchini humo.

Comments
Post a Comment