Mwandishi wetu
VIONGOZI wa klabu ya Simba, Rais Evans Aveva na Makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wataendelea kukaa gerezani baada ya kesi yao kutajwa leo na kuahirishwa hadi Agosti 16, mwaka huu kutokana na upande wa mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo imetajwa kwa mata ya tano, wawili hao wanakabiliwa na mashitaka matano yaliofunguliwa na akukuru ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) likiwemo la utakatishaji fedha, ambayo dhamana na wote wapo rumande gereza la Keko tangu Juni 29.
Kesi yao iko mbele ya Hakimu Victoria Nongwa ambaye baada ya upanda wa mashitaka kudau ushahidi haujakamilika, aliiihahirisha hadi Agosti 16, mwaka huu.
Mashitaka mengine wanayotumihumiwa nayo ni madai ya kughushi nyaraka zikionesha kuwa klabu inawalipa maden kiasi cha dola za Kimarekani 300,000.
Aveva anadaiwa kutoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, akiwa amekula njama na Kaburu kufanya uhalifu huo.
Kaburu anadaiwa kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano lina mhusisha pia la kutakatisha fedha kwa kumsadia Aveva katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.
Nafasi ya Aveva uraisi katika klabu ya Simba kwa sasa inakaimiwa na Salim Abdallah ‘Try Again’ huku Iddi Kajuna akikaimu umakamu wa Rais.

Comments
Post a Comment