![]() |
| Manchester United mabingwa msimu wa 2016-17 |
MONACO, Ufaransa
MAKUNDI ya Ligi ya Europa 2017-18 amepangwa mjini Monaco, Ufaransa , timu za timu za England, Arsenal, Liverpool na Everton zimejua wapinzani wake.
Katika mashindano hayo ambayo bingwa wake ni Manchester United, iliyopata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa kwa kutumia kofia hiyo, Gunners, iko tika Kundi H, itapambana na Bate Borisov ya Belarusia, Cologne na Red Star Belgrade.
![]() |
| Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp |
Arsenal inayonolewa na Arsene Wenger, haijafuzu Ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka 20, ni moja ya timu zinazopewa nafasi ya kutwaa ubingwa katika fainali itakayochezwa mjini Lyon, Ufaransa Mei mwakani.
Katika timu 48 na makundi 12, inajumuisha timu 16 ziliingia moja kwa moja, 22 zimetoka katika hatua ya mchujo na timu 10 zilizotolewa katika mchujo Ligi ya Mabingwa .
![]() |
| Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger |
Timu mbili za juu kwa kila kundi zitasonga mbele na kuunda timu 24 zitacheza hatua ya mtoano.
Yafuatayo ni makundi ya timu 12 ambapo kila moja lina timu nane yatakayochuana .
Kundi A: Villarreal (Hispania), Maccabi Tel-Aviv (Israel), Astana (Kazakhstan), Slavia Praha (Czech)
Kundi B: Dynamo Kyiv (Ukraine), Young Boys (Uswisi), Partizan (Serbia), Skenderbeu (Albania)
Kundi C: Sporting Braga (Ureno), Ludogorets (Bulgaria), Hoffenheim (Ujerumani), Istanbul Basaksehir (Uturuki)
Kundi D: AC Milan (Italia), Austria Vienna (Austria), Rijeka (Croatia), AEK Athens (Greece)
Kundi E: Lyon (Ufaransa), Everton (England), Atalanta (Italia), Apollon (Cyprus)
Kundi F: Copenhagen (DEN), Lokomotiv Moscow (Urusi), Sheriff (MDA), Zlin (Czech )
Kundi G: Victoria Plzen (Czech), Steaua Bucharest (Romania), Hapoel Beer-Sheva (Isreal), Lugano (Uswisi)
Kundi H: Arsenal (England), BATE Borisov (Bulgaria) Cologne (Ujerumani), Red Star Belgrade (Serbia)
Kundi I: Salzburg (Austria) Marseille ( Ufaransa) Vitoria SC (Ureno) Konyaspor (Uturuki)
Kundi J: Athletic Bilbao (Hispania), Hertha Berlin (Ujerumani), Zorya (Ukraine), Ostersund (Sweden)
Kundi K: Lazio (Italia), Nice (Ufaransa), Zulte Waregem (Ubelgiji), Vitesse (Uholanzi)
Kundi L: Zenit St Petersberg (Russia), Real Sociedad (Hispania), Rosenborg (Norway), Vardar (Macedonia)



Comments
Post a Comment