![]() |
| Ali Kiba |
Mwandishi wetu
BAADA ya kimya cha muda mrefu hatimaye mwanamuziki Ali Kiba ameachia wimbo mpya na kutuliza kio cha mashabiki wake.
Kiba ambaye akaunti yake ya Facebook inawafuasi zaidi ya milioni 2 ameachia wimbo wa mapenzi uitwao Seduce Me (Nitongoze Mimi) unaozungumzia mapenzi ambao mirindimo yake ni tofauti na ya nyimbo zake nyingine zilizotangulia, amejumuisha mipigo ya Charanga huku akitumia lugha ya kingereza, kihispaniola na kiswahili.
Katika video ya wimbo huo anaonekana akiwa na mrembo, akibusiana naye, akiwa naye kitandani huku akisema ma anamtaka amwambie ampigie na kuongeza (kwa sasa) ana majina mapya ambayo amepewa, mojawapo ni Kipusa.
Anasema anajua kupenda anagawa mavumba (fedha) na kama (mrembo huyo) anataka amwite Kiba Rock Star, Misifa,Unstoppable
Ana mandiga mapya kila mmoja anampa.
Pia anaonekana akiwa kitandani akichambua fedha (dola), na kujitokeza kisu, kisha kuzisunda katika bengi na kubeba bastola.
Wanaonekana warembo tofauti na mwisho kabisha mmoja wao anaonekana akivua pete na kuicha.

Comments
Post a Comment