![]() |
| Nassibu Abdul (Diamond Platnumz) na Ali Kiba (kulia). |
Mwandishi wetu
WASANII Ali Kiba na Nassibu Abdul na kundi lake la Wasafi Classic wameendelea kuvutana kwa nyimbo zao za Seduce Me na Zilipendwa kufuatiliwa na mashabiki wengi kwenye mtandao wa kijamii wa youtube huku kila mmoja ukitazamwa na mashabiki zaidi ya milioni 1.5
Hadi kufikia leo asubuhi, video ya wimbo wa Seduce Me wa Ali Kiba aliouachia kwenye mtandao siku tatu zilizopita, ili kuwaonjesha mashabiki wake, wa dakika 3:33, ulitolewa siku tatu zilizopita ulikuwa umetazamwa na mashabiki 1,827,888.
Mashabiki walio waliobonyeza alama ya kuupenda (like) ni 22,599 huku waliobonyeza alama ya kutopenda (dislike) ni 3,834.
Video hiyo imetazamwa na mashabiki wengi kwa muda mfupi, upo uwezekano idadi ya mashabiki watakaoutazama wakafikia zaidi ya milioni 2 leo.
Kwa upande wa video ya ya wimbo wa Zilipendwa wenye urefu wa dakika dakika 5:26 ulioimbwa Diamond kwa kushirikina na wasanii walio katika lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WBC), Harmonize, Rich Mavoko, Maromboso, Queen Darleen, Lavalava na Rayvanny ulio na siku mbili baada ya kuachiwa kwenye mtandao imetazamwa na mashabiki 1,153,338.
Mashabiki waliobonyeza alama ya kupenda wimbo huo uliotolewa siku moja baada ya Kiba kuachia Seduce Me ni 11,443 na kutopenda ni 4,079.
Nyimbo hizo zimekuwa zikipigwa sana na mashabiki wa kambi hizo mbili huku kila upande ukisifia ule wa msanii wake kuwa ni mkali zaidi.
Wafuatiliaji wa muziki wanasubiri kuona katika wiki moja idadi ya watazamaji wa nyimbo hizo itakuwaje, na kama wimbo wa Zilipendwa utatazamwa na watu wengi zaidi na kuwapita wa Seduce Me.
![]() |
| Ali Kiba (kulia) anavyoonekana katika moja ya sehemu za video ya Seduce Me |
Kiba ambaye akaunti yake ya Facebook inawafuasi zaidi ya milioni 2 ameachia Seduce Me (Nitongoze Mimi) unaozungumzia mapenzi ambao mirindimo yake ni tofauti na ya nyimbo zake nyingine zilizotangulia, amejumuisha mipigo ya Charanga huku akitumia lugha ya kingereza, kihispaniola na kiswahili.
Katika video ya wimbo huo anaonekana akiwa na mrembo, akibusiana naye, akiwa naye kitandani huku akisema ma anamtaka amwambie ampigie na kuongeza (kwa sasa) ana majina mapya ambayo amepewa, mojawapo ni Kipusa.
Anasema anajua kupenda anagawa mavumba (fedha) na kama (mrembo huyo) anataka amwite Kiba Rock Star, Misifa,Unstoppable
Pia anaonekana akiwa kitandani akichambua fedha (dola), na kujitokeza kisu, kisha kuzisunda katika bengi na kubeba bastola.
Wanaonekana warembo tofauti na mwisho kabisha mmoja wao anaonekana akivua pete na kuiacha.
Katika video Diamond na wasanii wenzie wanaonekana wamekiwa wamevaa mavazi ya zamani na kutumia ala za muziki wamewatumia wasanii waigizaji, kuendana na maneno yanayoimbwa kwenye wimbo huo.
![]() |
| Diamond Platnumz (wapili kushoto) na anavyonekana na wasanii wenzie katika video ya Zilipendwa. |
Wanaimba mapenzi ya zamani watu walikuwa wakipelekeana kadi na maua kuridhika , mtu kusema kuwa anampenda mwingine hadi kumwona kwenye glasi ya maji lakini kwa wanawake wa leo wanataka mikakati, ukiwa mzugaji huwapati.
Kuhusu mambo ya zamani waliyoyaimba kama ni zilipendwa ni kama kupiga chabo (kuchungulia ndani kupitia dirishani) na kutaja orodha watu walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kuachana ambapo katika kuonesha kuwa hawabagui pia ametajwa Diamond na Wema.
Kuhusu watu waliokuwa na hasama ambao wamebaki kama zilizopengwa wametajwa wengi ikiwemo, Bashite na Gwajima, pia mitindo ya muziki ya zamani kama bolingo, ndombolo, Chipolopolo, Simba wa Morogoro ( Afande Sele), MB Dog wa Latifah, Babu Tale Papa Misifa na hata pati watu hawaendi Kibisa imebaki zilipendwa.
Mpira na Pele zilipendwa, Dandu na Nyerere, Asha Ngedere, Arous Mabele, Idi Amini, masuala ya kuuza nyumba ili kuweka heshima baa nayo pia zilipendwa.
Mwishoni mwa wimbo huo wanaweza hata masualaya madili yaliyokuwepo enzi za Rais Kikwete sasa enzi za Magufuli imekuwa zilipendwa!
******



Comments
Post a Comment