Skip to main content

Cristiano Ronaldo aburutwa mahakamani







MADRID, Hispania
MWANASOKA nyota Cristiano Ronaldo leo ametinga katika mahakama nchini Hispania ambako anakabiliwa na mashitaka ya kukwepa mamilioni ya kodi .

Waendesha mashtaka wanamtuhumu Ronaldo ambaye ni manamichezo mwenye mapato makubwa zaidi duniani kukwepa kodi ya takribani dola milioni 17.3 (zaidi ya sh, bilioni 38.7).

Alitarajiwa kusema chochote baada ya kusomewa mashitaka lakini haikuwa hivyo.

Nyota huyo wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 32, awali alikanusha tuhuma hizo kwa kusema kuwa yeye ni mtu safi.

Ronaldo ni mwanasoka wa mwisho katika msururu wa wanasoka walioshitakiwa na mamlaka ya kodi ya Hispania.

Nyota wa Argentina,  Lionel Messi, anayeichezea Barcelona, alihukumiwa kifungo cha miezi 21 baada ya kukutwa na hatia ya kukwepa kodi mwaka jana.

Mwanzoni mwa mwezi huu, mahakama ilisema anaweza kulipa  euro 252,000 (zaidi ya sh. milioni 661.6) ili asifungwe.

Ronaldo alikaa mahakamani kwa muda wa saa moja na nusu, alitoa ushahidi kwa majaji wa mahakama ya Pozuelo de Alarcón iliyopo nje kidogo ya mji wa Madrid.

Waandishi wa vyombo vingi vya habari walikuwepo mahakamani kusubiri kumwona na kumpiga picha Ronaldo, lakini hawakuambulia kitu kutokana kuingia kwa kupitia njia ya chini inatokea gereji.

Wakati wa kutoka, Ronaldo alitarajiwa kuzungumza chochote lakini aliondoka kwenda nyumbani kwake moja kwa moja na kufanya baadhi ya waandishi kumzomea.

Kwa mujibu waendesha mashitaka, Ronaldo alikwepa kodi hiyo kwa kutumia muundo wa kampuni aliyoianzisha 2010 kuficha mapato yake na kodi aliyotakiwa kulipa  nchini Hispania yanayotokana na haki za kutumika kwa picha yake, kitu ambacho kinyume cha sheria.

Uongozi wa Ronaldo nao umekanusha madai hayo.

Akikutwa na hatia mshambuliaji huyo raia wa Ureno anaweza kutowa faini ya euro milioni 28 na kifungo cha miaka mitatu na nusu.

Comments

Popular posts from this blog

Wachezaji waliosajiliwa na kuhama timu zote Ligi Kuu England

WAKATI dirisha la usajili Ulaya 2017 lililoanza Juni 9 lNdaniafungwa leo saa sita usiku, ifuatayo ni orodha ya wachezaji walioingia na kutoka katika timu 20 za Ligi Kuu England . Kama wewe ni shabiki wa moja ya timu hizo angalia orodha hii ujue wachezaji walioingia au kuondoka. ARSENAL Ndani Alexandre Lacazette - Lyon (ada haijatajwa), Sead Kolasac - Schalke(bure). Nje Wojciech Szczesny - Juventus, pauni 14m, Gabriel Paulista - Valencia, pauni 10m, Kieran Gibbs - West Brom, pauni 7m, Yaya Sanogo - ameachwa, Stefan O'Connor - ameachwa, Kristopher da Graca - ameachwa,Kostas Pileas - ameachwa, Takuma Asano - Stuttgart- mkopo Chris Willock - Benfica, (ada haijatajwa), Glen Kamara - ameachwa, Marc Bola - Bristol Rovers- mkopo Carl Jenkson - Birmgham- mkopo Cohen Bramall - Birmgham- mkopo Emiliano Martiez - Getafe-mkopo, Stephy Mavididi - Preston-mkopo, Ismael Bennacer - Empoli, (ada haijatajwa), Jon Toral - Hull, (ada haijatajwa). BOURNEMOUTH Ndani Asmir Begovic - Ch...

Zidane ajuta kumtwanga kichwa Materazzi

Picha mbili tofauti zinazomwonesha  Zinedine Zidane alipofanya tukio la kumpiga kichwa Marco Materazzi . MADRID, Hispania KOCHA wa timu ya  Real Madrid Zinedine Zidane amekumbuka tukio alilofanya kwa kumpiga kichwa aliyekuwa mlinzi wa timu ya taifa ya Italia,  Marco Materazzi katika kipindi chake cha mwisho cha uchezaji akisema kuwa hajisikii kujivuna kutokana na tukio hilo. Zidane alifanya tukio hilo wakati akiichezea Real Madrid, wakati akiitumikia Ufaransa katika mechi ya fainali ya kombe la Dunia 2006 ambayo iliisha kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 kabla ya Azzuri kushinda kwa mikwaju ya penalti . Zidane ambaye alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Ufaransa katika kipindi cha Telefoot na kuoneshwa kwenye runinga, alisema anajutia tukio hilo alilofanya katika siku za mwisho kama mchezaji. "Sijisikii kujivunia," Zidane alisema.  Zinedine Zidane akioneshwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kichwa  Marco Materazzi. "Sijivunii tuk...

Wazazi 'wamsusa' mpenzi wa Ronaldo mjamzito

Cristiano Ronaldo akiwa na Georgina Rodriguez na mtoto wao Ronaldo Jr MADRID, Hispania MPENZI wa Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez anadaiwa kutengwa na wazazi wake. Mrembo huyo mwenye  umri wa miaka 23 anatarajia kujifungua mtoto wa kike Oktoba mwaka huu na kuongeza familia familia yake na Ronaldo inayokuwa kwa  haraka,  lakini kuna taarifa mama na baba yake hawajihusishi katika ujauzito huo. Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Hispania, Rodriguez hamekuwan hana uhusiano mzuri na wazazi wake. Limeripoti kuwa kutokana na baba yeke Jorge Eduardo Rodriguez kuishi Argentina, na mama yake, Ana Maria Hernandez yuko nchini Italia, anamaliza kipindi chake cha ujauzito bila ya kupata sapoti. Mwanamitindo huyo mwenye damu mchanganyiko ya Kihispania na ki-Argentina mzaliwa wa Jaca kaskazini mashariki mwa Hispania, amebakia  katika nchi aliyozaliwa na sasa yuko na nyota wa Real Madrid ,anarajia kupata mtoto ambaye atakuwa wa nne kwa Ronaldo. Mtoto atakayemza...